TETESI za usajili zinasema Manchester United inahangaika kusaka mrithi sahihi wa kiungo mkabaji Carlos Henrique Casimiro maarufu Casemiro, ambaye imekuwa kijaribu kumuuuza kufuatia kufanya vibaya msimu wa 2023/24 na sasa inajiandaa kwa msimu mpya ikimfikiria.
Mashetani hao wekundu pia wanasota kukubaliana vipengele na Paris Saint-Germain kuhusu dili la kumsajili Manuel Ugarte. (GiveMeSport)
SOMA: Casemiro, Fred wajiangalie leo
Arsenal itaendelea na mpango wake wa kumsajili kiungo wa Real Sociedad, Mikel Merino mara baada ya uhamisho wa Emile Smith Rowe kwenda Fulham kukamilika. (Football Transfers)
Rais wa Real Sociedad, Jokin Aperribay amekiri klabu hiyo itakubali ofa kwa ajili ya Merino, ambaye pia anawindwa na Barcelona, iwapo ataiambia klabu anataka kuondoka. (MARCA – Spain)
Liverpool imewasilisha ombi la pauni milioni 21 katika klabu ya Genoa kwa ajili ya kumsajili kiungo Morten Frendrup, lakini timu hiyo ya Italia haina nia kumuuza mchezaji huyo. (TuttoMercatoWeb – Italy)