Rais Samia atunukiwa Shahada ya Heshima Nigeria

DODOMA – Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima kutoka Nasarawa State University, Keffi nchini Nigeria, kupitia hafla iliyofanyika kwa njia ya mtandao Aprili 11, 2026.

Hafla hiyo imefanyika Ikulu ya Dodoma, ambapo Rais Samia alipokea heshima hiyo inayotambua mchango wake katika uongozi, maendeleo na masuala ya kijamii barani Afrika.

Kwa mujibu wa chuo hicho, Rais Samia ametunukiwa shahada hiyo kwa kutambua nafasi yake kama kinara wa nishati safi ya kupikia, juhudi zake katika kuboresha afya ya mama na mtoto, pamoja na mchango wake katika kuimarisha taswira ya uongozi wa wanawake barani Afrika.

Aidha, chuo hicho kimetambua juhudi zake katika kusimamia na kuendeleza masuala ya biashara, hususan kwa vijana, kama sehemu ya mkakati wa kukuza uchumi jumuishi na fursa za ajira.

Tuzo hiyo inaongeza orodha ya heshima za kimataifa zinazotolewa kwa Samia Suluhu Hassan, huku ikiakisi mchango wa Tanzania katika ajenda za maendeleo endelevu, usawa wa kijinsia na uongozi barani Afrika.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

  2. I get paid over $130 1 to 3 hours working from home with 2 kids at home. I never thought I’d be able to do it but my best friend earns over $27k a month doing this and she convinced me to try. The potential with this is endless.
    Heress——-> http://www.giftpay7.vip

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button