Ilkay Gündoğan arejea Man City
KIUNGO Ilkay Gündoğan amejiunga tena na Manchester City mwaka mmoja tu baada ya kuondoka klabu hiyo kwenda kuitumikia Barcelona.
Habari zimesema kiungo huyo amesaini mkataba wa awali wa mwaka mmoja Etihad huku Barca ikimruhusu kuondoka kwa uhamisho huru.
Wakati jezi yake ya awali namba 8 sasa inavaliwa na Mateo Kovacic, Gündoğan atavaa jezi namba 19 msimu huu.
SOMA: Gundogan akubali kurejea Barcelona
Gündoğan ameiambia mitandao ya habari ya City:”Miaka yangu saba Manchester City ilikuwa wakati wa furaha kuu kwangu, ndani na nje ya uwanja.”
Gündoğan amecheza vilabu kadhaa Ulaya ikimwemo 1. FC Nürnberg ya Ujerumani aliyojiunga nayo mwaka 2009 kabla ya kusaini Borussia Dortmund mwaka 2011, akishinda Bundesliga na Kombe la Ujerumani msimu wa 2011/2012.