Gundogan akubali kurejea Barcelona
IMERIPOTIWA kiungo wa Barcelona, Ilkay Gundogan amekubali kurejea Manchester City.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo kutoka Italia, Fabrizio Romano Barcelona inataka kumuachia na Mjerumani huyo yupo tayari kuondoka, hata hivyo Guardiola tayari ameonesha kumtaka.
SOMA: Fahamu Guardiola anavyompa majukumu Bernado
Taarifa ya BBC imeleeza kuwa licha ya kuwa na mkataba wa miaka miwili, Barcelona haitakuwa na kipingamizi endapo mchezaji huyo atataka kuondoka.
View this post on Instagram
Gundogan alijiunga na vijana wa Camp Nou msimu uliopita ambapo alisaini miaka mitatu.
.Gundogan pia amepata ofa kutoka baadhi ya klabu za Qatar na Saudia.