Islam Huwel aibuka Iringa Mjini, aahidi mapinduzi ya kiuchumi

IRINGA: Mjasiriamali na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Islam Huwel, leo amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia chama hicho, akiahidi kuufanya mji huo kuwa kitovu cha biashara na ajira kwa vijana.

Huwel amesema dhamira yake ni kuhakikisha vijana wa Iringa wanapata elimu ya ujasiriamali na kuunganishwa kwenye mnyororo wa thamani wa biashara, ili kupunguza utegemezi na kuongeza kipato chao.

“Ni wakati wa kuuchangamsha mji wa Iringa kibiashara.

Tutafungua milango ya fursa, tutasaidia wajasiriamali wadogo na kuhakikisha huduma bora za kijamii zinawafikia wananchi wote,” amesema.

Ameeleza pia kuwa atapigania kuboreshwa kwa sekta za afya, elimu, maji na miundombinu, sambamba na kuvutia wawekezaji watakaoongeza thamani ya uchumi wa Iringa kwa ujumla.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button