Kafulila kuongoza mdhahara nafasi ya PPP katika maendeleo

ARUSHA: Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP Centre) kinatarajiwa kufanya mhadhara wa umma utakaolenga kujadili mchango wa ubia kati ya sekta umma na sekta binafsi katika kuchochea maendeleo ya watu na uchumi wa taifa.

Mhadhara huo utaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa PPP Centre, David Kafulila ukiwa umebeba mada ya “Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kama Nyenzo ya Kuchochea Maendeleo ya Watu: Fursa katika Mpango wa Nne wa Maendeleo (FYDP IV) na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.”

Mhadhara huo unatarajiwa kufanyika Agosti 14, asubuhi katika ukumbi wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru(TICD) jijini Arusha, na unatarajiwa kuwahusisha wanafunzi, wahadhiri na wadau kutoka sekta ya umma, sekta binafsi pamoja na washirika wa maendeleo.

Aidha, mhadhara huo unalenga kuongeza uelewa kuhusu nafasi ya ubia wa PPP katika kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuvutia uwekezaji na kuchochea ukuaji wa uchumi unaowanufaisha wananchi, sambamba na malengo ya FYDP IV na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily…………
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button