Kompany ajipa matumaini jereha la Kane

KOCHA wa Bayern Munchen, Vincent Kompany anatumai kuwa jeraha la kifundo cha mguu la mshambuliaji, Harry Kane sio mbaya kwa kiwango kikubwa.

Kane,31, alipata jeraha hilo katika mchezo wa jana dhidi ya Bayer Leverkusen ulioisha kwa sare ya 1-1 uwanja wa Allianz Arena, mjini Munich.

Mwingereza huyo alitolewa dakika ya 86 baada ya kufanyiwa madhambi na mchezaji Amine Adli wa Leverkusen.

Advertisement

Kikosi cha Kompany kitasafiri kumenyana na Aston Villa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Jumatano.

“Mimi si daktari, lakini natumai sio jambo zito. Bado ni mapema kusema. Tunatumai atakuwa fiti Jumatano,” Kompany alisema mara baada ya mchezo huo.

Katika mchezo huo wa Bundasliga, Bayer Leverkusen waliaanza kuandika bao dakika ya 31 lililofungwa  na Robert Andrich, kasha dakika nane baadaye Aleksandar Pavlović kusawazisha na mchezo kuisha sare.