Mchengerwa aagiza utambuzi wenye uhitaji maalum
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amewaagiza wakuu wa mikoa ,wilaya pamoja na viongozi wa halmashuri zote nchini kusimamia zoezi la ubainishaji na utambuzi wa awali wa watoto wenye mahitaji maalum.
Mchengerwa amesema inatakiwa kuundwa mikakati ya kuwalinda wenye ulemavu wa ngozi ili kudhibiti matukio ya mbalimbali ya ukatili wanayofanyiwa.
Mchengerwa ametoa agizo hilo leo jijiji Arusha wakati wa kufungua Maadhimisho ya miaka 30 ya Elimu Jumuishi yanayofanyika shule ya Elimu Jumuishi ya Patandi iliyopo wilayani Arumeru.
Maadhimisho hayo yamejumuisha watoto wenye mahitahi maalum kutoka shule mbalimbimbali ikiwemo maofisa elimu sekondari na msingi pamoja na wadau wa elimu hiyo jumuishi.
Alisema zoezi la kubaini watoto hao wenye mahitaji maalum lifanyike kabla ya kipindi cha uandikishaji kwa kufuata miongozo ya utekelezaji wa zoezi hilo iliyotolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI mwaka 2022 na ile iliyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2023,
“Ma Rc ,Dc na viongozi wa halmashauri anzeni zoezi la kuhakikikisha watoto wenye ulemavu wanatolews nyumbani na kwenda shule na wale wanaowaficha watoto hawa wabainike lakini wanaofanya ukatili kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wachukuluwe hatua mara moja,” amesema Mchengerwa.