• Kuhusu HabariLEO
  • Matangazo: Maelekezo & Bei
  • Nunua E-Paper
HabariLeo
No Result
View All Result
No Result
View All Result
HabariLeo
No Result
View All Result

Mil 3/- kushindaniwa kombe la mbunge Missenyi

Diana Deus by Diana Deus
April 21, 2025
in Michezo na Burudani
0
Mil 3/- kushindaniwa kombe la mbunge Missenyi

JUMLA ya Sh milioni 3 zinashindaniwa katika mashindano ya mpira wa miguu yaliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Nkenge Wilaya Missenyi mkoani Kagera ambayo yatashirikisha timu 20 kutoka katika wilaya hiyo.

Mashindano hayo yenye jina la Dk Samia na Kyombo yanalenga kuwakunsanya vijana wa  Missenyi ili kuibua vipaji vya vijana wanaoishi vijiji vya pembezoni mwa Tanzania na kiviendeleza katika ngazi nyingine za mpira wa miguu chini pamoja na kuendeleza mshikamano kutoka kwa vijana wa kata moja hadi nyingine.

Mashindano hayo yamefunguliwa rasmi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa katika Uwanja wa Mashujaa, Bunazi, wilayani Missenyi, mkoani Kagera, na yanatarajiwa kutamatika Juni.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Bashungwa amesema kuwa mashindano hayo yatasaidia kuibua vipaji vya michezo kwa vijana, kuimarisha afya, kuendeleza mshikamano na kudumisha upendo miongoni mwa vijana na wakazi wa Wilaya ya Missenyi huku watakaonyesha vipaji vyao watapata nafasi ya kutafuta fursa nyingine za kimichezo ndani na nje ya nchi.

“Mbunge kwa kushirikiana na Madiwani wameonyesha dhamira ya dhati katika maendeleo ya michezo ndani ya Wilaya ya Missenyi ligi hii siyo tu burudani bali pia ni fursa kwa vipaji chipukizi,wilaya hii Iko pembezoni lakini naelewa kuwa vijana wengi wanavipaji hivyo wasisite kuonyesha vipaji vyao ,naomba vijana kutoka kata zote 20 mshiriki kwa moyo wa upendo na mshikamano,” amesema Bashungwa.

Aidha, Waziri Bashungwa ametoa wito kwa waamuzi na wasimamizi wa mashindano hayo kuhakikisha wanatenda haki wakati wa michezo yote, katika mashindano hayo ili kiyafanya yamalizike kwa amani na kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

Mbunge wa Jimbo la Missenyi, Florent Kyombo, alisesema kuwa mashindano hayo yanalenga kuimarisha mahusiano na mshikamano kati ya vijana na wananchi wa kata zote 20 za wilaya hiyo na hiyo ilikuwa moja ya haadi zake katika kuhakikisha anatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ni lazima vijana wapate fursa ya kushiriki michezo na kuonyesha vipaji vyao.

Amesema kuwa viwanja vya Mugana B na uwanja wa Mashujaa Bunazi ndivyo vitakavyotumika katika mashindano hayo kwa kukutanisha makundi yaliyopangwa na kamati.

Hafla ya uzinduzi ilizikutanisha timu za kata za Kyaka na Mtukula, timu zote shiriki zilipatiwa vifaa mbalimbali vya michezo, ikiwemo jezi, mipira, vifaa vya mazoezi, pamoja na fedha kwa ajili ya maandalizi ya mechi.

Previous Post

Rais Samia atuma salamu kifo cha Papa Francis

Next Post

Machinga, bodaboda Dar wagomea maandamano Chadema

Next Post
Machinga, bodaboda Dar wagomea maandamano Chadema

Machinga, bodaboda Dar wagomea maandamano Chadema

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Zilizosomwa Ziadi

  • Mradi mpya kupunguza msongamano bandari ya Dar
    Mradi mpya kupunguza msongamano bandari ya Dar
  • Kairuki apongeza upanuzi  huduma za intaneti
    Kairuki apongeza upanuzi huduma za intaneti
  • Mbegu bora, chachu ya kilimo cha ushindani
    Mbegu bora, chachu ya kilimo cha ushindani
  • Luizer ampongeza Asha Baraka
    Luizer ampongeza Asha Baraka
  • Luizer awasihi wanawake kutunza ngozi
    Luizer awasihi wanawake kutunza ngozi

Latest on this theme

  • (no title)
    by Yohana Shida, Geita
    September 5, 2022
  • (no title)
    by NEW YORK, Marekani
    September 6, 2022

  • Kuhusu HabariLEO
  • Matangazo: Maelekezo & Bei
  • Nunua E-Paper

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

No Result
View All Result

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.