Miradi ya bil 18/- kupitiwa na mwenge uhuru Shinyanga

SHINYANGA: MKOA wa Shinyanga umeupokea Mwenge wa Uhuru ambao utapitia, kuzindua na kuweka Jiwe la Msingi miradi 45 yenye thamani ya Sh bilioni 18.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, ameeleza hayo leo Agosti 18, 2026 alipoupokea mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda katika eneo la Shule ya Msingi Mwigumbi iliyopo wilayani Kishapu.
Mhita amemueleza kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Wazo Mwang’onda kuwa utakimbizwa kilomita 739.2 katika wilaya tatu za Shinyanga, Kishapu na Kahama.

Miradi 13 yenye thamani ya Sh bilioni 12 itawekwa mawe ya msingi, miradi 17 itazinduliwa yenye thamani ya Sh bilioni 4.2 na miradi minne itakaguliwa yenye thamani ya Sh milioni 375 na miradi 11 yenye thamani ya Sh bilioni 1.4 itaonwa, itakaguliwa na kupandwa miti.

Hara hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Peter Masindi amepokea mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita ambapo ameeleza utapitia miradi nane yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 1.8 ambapo miradi mitano itazinduliwa ,mmoja utafunguliwa,mmoja utakabidhiwa na mmoja utawekewa jiwe la msingi.
Masindi amesema kwa wilaya hiyo utakimbizwa kilomita 128.7 ikiwemo ofisi ya mtendaji wa kijiji cha Songwa imewekwa jiwe la msingi na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa.



