BAADA ya sare mbili tasa za michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, klabu ya Azam leo inashuka uwanjani dhidi ya wenyeji KMC kwenye uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam katika mchezo pekee wa ligi hiyo.
Azam ilitoka suluhu dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kwenye uwanja wa Mej Jenerali Isamuhyo Agosti 28 kabla ya suluhu nyingine dhidi ya Pamba kwenye uwanja wa Azam Complex Septemba 14.
SOMA: Pazia Ligi Kuu bara kufunguliwa leo
KMC ipo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 4 baada ya michezo 3 wakati Azam inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 2 baada ya michezo 2.
Singida Black Stars inaongoza Ligi Kuu ikiwa na pointi 12 baada ya michezo 4 wakati KenGold inashika mkia nafasi ya 16 haina pointi baada ya michezo 3.