Pazia Ligi Kuu bara kufunguliwa leo

MSIMU mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 unaanza leo kwa mchezo mmoja wa ufunguzi kufanyika jijini Mwanza.

Pamba Jiji baada ya kurejea Ligi Kuu itaanza kampeni kusaka ubingwa dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

SOMA: Bado vibali tu, VAR kutumika Ligi Kuu

Pamba iliyoshuka daraja miaka 20 iliyopita imepanda tena pamoja na klabu ya Kengold ya Mbeya.

Bingwa mtetezi wa Kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara ni Yanga iliyolitwaa mara 30 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo yenye makao yake Kariakoo, Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

Back to top button