• Kuhusu HabariLEO
  • Matangazo: Maelekezo & Bei
  • Nunua E-Paper
HabariLeo
No Result
View All Result
No Result
View All Result
HabariLeo
No Result
View All Result

DStv, SuperSport Kurusha ‘Live’ Mechi Zote 104 za Kombe la Dunia 2026

Mwandishi Wetu by Mwandishi Wetu
April 18, 2026
in Michezo na Burudani
4
DStv, SuperSport Kurusha ‘Live’ Mechi Zote 104 za Kombe la Dunia 2026

DAR ES SALAAM: KAMPUNI ya matangazo ya michezo ya SuperSport kwa kushirikiana na DStv imetangaza kuwa itarusha mubashara mechi zote 104 za FIFA World Cup 2026, mashindano yatakayofanyika katika nchi za Mexico, Canada na Marekani.

Tangazo hilo limetolewa na kampuni hiyo, ambayo ni tanzu ya MultiChoice Group chini ya CANAL+, ikieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuwapa watazamaji barani Afrika fursa ya kushuhudia moja kwa moja mashindano hayo makubwa zaidi katika historia ya soka.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kwa mara ya kwanza wateja wote wa DStv kuanzia kifurushi cha Access hadi Premium wataweza kufuatilia mechi zote mubashara, pamoja na vipindi vya muhtasari na marudio, hatua inayopanua upatikanaji wa mashindano hayo kwa hadhira kubwa zaidi.

Michuano ya Kombe la Dunia 2026 imepanuliwa kutoka mataifa 32 hadi 48 na inatarajiwa kuanza Juni 11, 2026 jijini Mexico City na kuhitimishwa Julai 19, 2026 katika jiji la New Jersey, ikiwa ni toleo lenye mechi nyingi zaidi kuwahi kufanyika.

Katika kuonesha uzito wa tukio hilo, Idris Elba alishiriki kutangaza kuwa mechi zote 104 zitarushwa mubashara kupitia DStv, akiwakilisha uhusiano wa Afrika na jukwaa hilo la kimataifa.

Kwa upande wa bara la Afrika, jumla ya mataifa 10 yamefuzu kushiriki mashindano hayo kupitia Shirikisho la Soka Afrika (CAF), likiwa ni idadi kubwa zaidi kuwahi kutokea. Mataifa hayo ni pamoja na Ghana, Senegal, Morocco, Misri na Afrika Kusini, miongoni mwa mengine.

Akizungumza kuhusu maandalizi hayo, Mkurugenzi wa CANAL+ anayehusika na maudhui na michezo katika Afrika inayozungumza Kiingereza na Kireno, Rendani Ramovha, amesema kampuni hiyo inalenga kuleta uzoefu wa hali ya juu wa utazamaji kwa Waafrika.

Amesema kuwa ushiriki mkubwa wa mataifa ya Afrika unaongeza mvuto wa mashindano hayo, huku akibainisha kuwa vipindi maalum vya uchambuzi na maudhui yatakayozingatia tamaduni za Kiafrika vitaandaliwa ili kuboresha uzoefu wa watazamaji.

Huduma ya matangazo ya Kombe la Dunia 2026 kupitia SuperSport itapatikana katika nchi zaidi ya 25 barani Afrika, ikiwemo Tanzania, Kenya, Nigeria na Afrika Kusini.

Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa ushiriki wa watazamaji wa Afrika katika mashindano hayo, pamoja na kuimarisha nafasi ya SuperSport kama mtangazaji kinara wa michezo barani Afrika.

Previous Post

Mwigulu ataka uwanja wa AFCON 2027 ukamilike kwa wakati

Next Post

Viongozi wa dini, siasa waaga miili waliokufa mvua

Next Post
Viongozi wa dini, siasa waaga miili waliokufa mvua

Viongozi wa dini, siasa waaga miili waliokufa mvua

Comments 4

  1. Mirriam Barret says:
    4 months ago

    Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

    Reply
  2. Mirriam Barret says:
    4 months ago

    Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills requihred for this job andh regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

    Reply
  3. DavidTMayfield says:
    4 months ago

    I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..    https://www.work27.info

    Reply
  4. Marinda Strudwick says:
    4 months ago

    Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

    Reply

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Zilizosomwa Ziadi

  • Mradi mpya kupunguza msongamano bandari ya Dar
    Mradi mpya kupunguza msongamano bandari ya Dar
  • Kairuki apongeza upanuzi  huduma za intaneti
    Kairuki apongeza upanuzi huduma za intaneti
  • Mbegu bora, chachu ya kilimo cha ushindani
    Mbegu bora, chachu ya kilimo cha ushindani
  • Luizer ampongeza Asha Baraka
    Luizer ampongeza Asha Baraka
  • Luizer awasihi wanawake kutunza ngozi
    Luizer awasihi wanawake kutunza ngozi

Latest on this theme

  • (no title)
    by Yohana Shida, Geita
    September 5, 2022
  • (no title)
    by NEW YORK, Marekani
    September 6, 2022

  • Kuhusu HabariLEO
  • Matangazo: Maelekezo & Bei
  • Nunua E-Paper

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

No Result
View All Result

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.