Watanzania wang’aa mbio za Tanfoam

ARUSHA: WANARIADHA kutoka Tanzania wamefanikiwa kung’ara katika mashindano ya kimataifa ya mbio ndefu za Tanfoam baada ya kumaliza washindi kwa kilometa 42 na kilometa 21 kwa wanawake na wanaume.
Katika mbio ndefu za kilometa 42 mwanariadha Modest Kalist kutoka klabu ya Ambassador Arusha aliongoza kwa muda wa saa 2:15:58, nafasi ya pili ilishikiliwa na mwanariadha kutoka Kenya Mosses Mengich kwa Muda wa saa 2:20:02 huku Uganda ikishika nafasi ya tatu kwa mwanariadha wake Akankwasa Jonathan kwa muda wa saa 2:20:23.

Kwa wanawake. Kilometa 42 Vaileth Adam kutoka klabu ya talent Arusha alishinda kwa muda wa saa 2:42:10, akifuatiwa na Maureen Jepkohech kutoka Kenya kwa muda wa saa 2:43:19 huku nafasi ya tatu kuwa ni mwanariadha Edna Too kutoka Kenya aliyetumia muda wa saa 2:44:16.
Katika Mbio za Kilomita 21 Wanaume Boay Maganga Mwanariadha kutoka talent klabu alishinda kwa muda wa saa 1:04:50 akifuatiwa na Protas Gabriel kutoka Singida kwa muda wa saa 1:05:04.

Kwa wanawake kilometa 21 wanawake , Magdalena Shauri kutoka JWTZ alishinda kwa muda wa saa 1:11:36 .
Kwa kilometa 10,Sisilia Gonoka kutoka JWTZ muda wa na wanaume Inyas Sulle kutoka JWTZ muda wa dakika 30:03.
Mkuu wa kitengo cha mauzo kampuni ya Tanfoam Glorious Temu ambaye pia ni mwenyekiti wa mbio amesema ni Msimu wa pili zimefanyika ,lengo ni kuhamasisha michezo na kurudisha kwa jamii katika kusaidia makundi mbalimbali yenye uhitaji ambapo amewashukuru wadhamini wote pamoja na washiriki kushiriki na kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii na sasa wanajipanga kwa mbio ijayo ya 2027.

Amesema mbio hizo zimefanyika katika kuelekea kutimiza miaka 60 ya Tanfoam mwaka huu ikiwa ni tangu kuanzishwa kwake na mwaka huu zaidi ya washiriki 1000 walishiriki ambapo zawadi nono za fedha na bidhaa za Tanfoam zimetolewa kwa washindi mbalimbali .
Naye Mgeni rasmi Cosmas SADATI Meneja wa CRDB benki kanda ya kaskazini amesema wanariadha wa Tanzania wamepambana na kuwashinda kutoka nje ya nchi na hii inaonyesha kuwa kazi kubwa inafanyika katika mchezo huu hapa nchini.
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Rogath Steven ameeleza mbio sasa imekuwa ya kimataifa na sasa zimewekwa katika kalenda ya shirikiko la Riadha Afrika pamoja na Dunia na hii ni baada ya kutimiza vigezo vyote na ndio maana wanariadha kutoka nchi za Kenya na Uganda wameweza kushiriki.
” Mbio zimekuwa chachu katika unatambua mchango wa waandaaji wa mbio na waendelee kufuata kanuni na taratibu zilizopo na baadhi wamekuwa hawafuati hatutasita kuwachukulia hatua,” ameongeza.



