Mwandishi Habarileo ashinda tuzo ya korosho
DODOMA: MWANDISHI wa Habari wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) anayeandikia gazeti la HabariLeo mkoani Mtwara, Sijawa Omary leo ameshinda tuzo ya uandishi bora wa habari za korosho.
Sijawa ameshinda tuzo hiyo katika mfumo wa kuteuliwa na kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Newala mkoani Mtwara, Rajabu Kundya katika mkutano mkuu wa siku mbili wa wadau wa tasnia ya korosho mwaka 2024 uliyofanyika Dodoma.
Tuzo hiyo imetolewa na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Kwa lengo la kutambua mchango mkubwa wa TSN.
MWANDISHI wa Habari wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) anayeandikia gazeti la HabariLeo mkoani Mtwara, Sijawa Omary leo ameshinda tuzo ya uandishi bora wa habari za korosho. pic.twitter.com/yaCel7SXyi
— HabariLeo (@HabariLeo) August 23, 2024