MICHEZO miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara inapigwa leo Mwanza na Mbeya ikihusisha timu za majeshi dhidi ya majiji.
Baada ya kutoka sare dhidi ya Fountain Gate katika mchezo uliopita kwenye uwanja a Tanzanite, Kwaraa Babati, Dodoma Jiji leo itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
SOMA: Kivumbi ‘derby’ ya majiji Ligi Kuu leo
Dodoma Jiji ipo nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 5 baada ya michezo 4 wakati Prisons inashika nafasi ya 11 ikiwa na pointi 3 baada ya michezo 3.
Nayo Pamba Jiji ambayo ilipoteza mechi iliyopita kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 nyumbani dhidi ya Singida Black Stars, itakuwa mwenyeji wa maafande wa Mashujaa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mashujaa ipo nafasi ya 3 ikiwa na pointi 7 baada ya michezo 3 wakati Pamba Jiji inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 3 baada michezo 4.