Kivumbi ‘derby’ ya majiji Ligi Kuu leo
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili kupigwa Mwanza na Kagera.
Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Mashujaa, Dodoma Jiji itakuwa mgeni wa Pamba Jiji kwenye uwanja CCM Kirumba jijini Mwanza.
SOMA: Pazia Ligi Kuu bara kufunguliwa leo
Kivumbi kingine kitakuwa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wakati wenyeji Kagera Sugar itakapokiwasha dhidi ya Singida Black Stars.
Huo ni mchezo wa kwanza kati ya timu hizo Ligi Kuu baada ya iliyokuwa Ihefu kubadilishwa jina na kuitwa Singida Black Stars.
Katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Februari 25, 2024 kwenye uwanja wa Kaitaba wakati huo Singida Black Stars ikiitwa Ihefu, Kagera Sugar ilishinda kwa mabao 2-1.