Miradi ya gesi Mtwara yaikosha kamati ya Baraza la Wawakilishi

DODOMA: Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Uchumi na Uwekezaji Zanzibar imeeleza kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya gesi asilia mkoani Mtwara.
Hayo yameelezwa Aprili 16, 2026 wakati wa ziara iliyoratibiwa na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kwa lengo la kuongeza uelewa kwa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu shughuli za utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa gesi asilia.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Makame Sufiani alibainisha kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya kazi kubwa kuwekeza katika miundombinu ya gesi asilia, hatua iliyoleta manufaa makubwa kwa Taifa.
“Tumeridhishwa na kazi kubwa inayofanyika hapa Mtwara. Huu ni mfano mzuri wa namna rasilimali za Taifa zinavyoweza kusimamiwa kwa tija na kuwanufaisha wananchi,” alisema Sufiani.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Mboja Mshenga, ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanza hatua za awali za ukusanyaji taarifa za petroli za mfumo wa 3D zitakazowezesha kubaini uwepo wa gesi asilia na mafuta visiwani humo.
SOMA: Wizara, PURA waweka mikakati utafitaji mafuta, gesi asilia
“Tumeanza hatua za msingi za utafiti ili kufungua fursa za uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi, jambo litakalosaidia kukuza uchumi wa Zanzibar na kuongeza mapato ya Serikali,” alisema.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PURA, Halfani Halfani, amesema ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Hati ya Mashirikiano iliyoingiwa kati ya PURA na Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta Zanzibar (ZPRA) mwaka 2022.
Ameeleza ushirikiano huo unawapa fursa ya kubadilishana uzoefu wa kiufundi na kitaalamu katika usimamizi na udhibiti wa shughuli za utafutaji, uendelezaji na uzalishaji mafuta na gesi asilia.
Amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza ufanisi wa sekta hiyo na kuhakikisha kuwa rasilimali hizo zinatumika kwa manufaa ya wananchi.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site