Onesho mtoto wa mutukudzi kivutio Zanzibar

MTOTO wa gwiji wa muziki wa Afrika, Hayati Oliver Mutukudzi, Selmor Mutukudzi imekuwa livutio katika Tamasha la Sauti za Busara linaloendelea viunga vya Ngome Kongwe ndani ya Ukumbi wa Mambo Club Unguja, Zanzibar.

Selmor Mutukudzi ambaye alipanda jukwaani na bendi yake, alianza shoo yake kwa kibwagizo cha wimbo wa marehemu baba yake wimbo wa ‘Neria’ na ‘Todii’ ambavyo viliamsha shangwe kwa mashabiki wengi walioudhulia uzinduzi wa tamasha hilo.

Selmor Mutukudzi amesema kutumbuiza katika tamasha hilo ilikiwa ni sehemu ya ndoto yake kubwa.

Advertisement

‘’Nimekuwa, nikiomba kushiriki Sauti za Busara, muda mrefu ila sikufanikiwa. Nashukuru kwa mwaka huu nimepata nafasi na mashabiki wamenifurahia,” amesema.

Selmor Mutukudzi kipaji chake kilioneka tokea akiwa na miaka 10, baada ya baba yake kumfundisha muziki na ana albamu sita ikiwemo inayoitwa ‘Shungu’ aliyoitoa mwaka 2008.