Pauni mil 21 kumpeleka Joao Cancelo Al-Hilal

KLABU ya Manchester City imefikia makubaliano na timu ya Al-Hilal inayoshiriki ligi ya kulipwa Saudi Arabia kumuuza beki Joao Cancelo kwa pauni million 21.2.

Habari zimesema vipengele binafsi havifikiriwi kuwa tatizo dili hilo ingawa bado Cancelo hajakubali uhamisho huo.

Iwapo atakubali, Cancelo mwenye umri wa miaka 30 anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu hivyo kumaliza kumaliza mitaka mitano ya kuwepo Etihad.

SOMA: Barcelona yang’ang’ana kwa João Cancelo

Mwezi huu Kocha wa City Pep Guardiola alisema Cancelo anaweza kucheza klabu hiyo tena.

Hata hivyo, mvutano uliosababisha Cancelo kutumikia Bayern Munich na Barcelona kwa mkopo kwa zaidi ya miezi 18 huenda ukawa kikwazo kikubwa.

Cancelo hajacheza michezo miwili ya City ya Ligi Kuu Englang msimu huu.

Pia hakucheza mechi City ilipotwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii kwa kuifunga Manchester United.

Awali, beki huyo wa Ureno alikuwa beki wa pembeni wa kwanza wa Guardiola aliyeingia katikati, lakini baadaye alipoteza nafasi yake miezi michache tu baada ya kusaini mkataba mpya mwaka 2022.

Manchester City ililipa pauni milioni 60 kumsajili Joao Cancelo kutoka Juventus mwaka 2019.

Habari Zifananazo

Back to top button