TETESI za usajili zinasema Barcelona inataka kumsajili tena João Cancelo toka Manchester City kufuatia mkopo wenye mafanikio msimu uliopita.
Lakini beki wa Manchester United, Aaron Wan-Bissaka yupo katika orodha ya mbadala iwapo Barca itashindwa kumsajili mlengwa mkuu wake huyo nafasi ya beki wa kulia. (Caught Offside)
Manchester United imetoa ofa ya mkataba wa miaka mitano kwa Matthijs de Ligt, huku mazungumzo yakiendelea na Bayern Munich kuhusu ada ya uhamisho kwa ajili ya beki huyo wa Uholanzi.(De Telegraaf – Netherlands)
Arsenal imekamilisha rasmi usajili wa kudumu wa pauni mil 27 wa David Raya baada ya kipindi cha mkopo kutoka klabu ya Brentford kumalizika. (Daily Mail)
Newcastle United ina uhakika itaweza kumbakisha Alexander Isak licha ya ongezeko la nia ya kumsajili kutoka Chelsea. (Football Insider)
Liverpool ni miongoni mwa timu ambazo zinaweza kutoa ofa ya mkataba kwa kiungo huru Adrien Rabiot. AC Milan pia inatafakari kutoa ofa. (Calciomercato – Italy)
Liverpool pia huenda ikajaribu tena kumsajili Anthony Gordon kutoka Newcastle baada ya mazungumzo wiki iliyopita kutozaa matunda.(TEAMtalk)