Rais Samia: Mmeitangaza vyema Tanzania

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema nidhamu, juhudi na kujituma ndiyo nguzo ya mafaniko ya Fadhili na Ibrahim (The Ramadhani Brothers) ambao usiku wa leo wameshinda tuzo ya American Got Talent Fantasy League 2024 na kujizolewa Dola 250,000 sawa na zaidi ya Sh milioni 600.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Februari 20, 2024 katika andiko lake la pongezi kwenye mtandao wa X na kuongeza kuwa ushindi huo unaitangaza Tanzania na kuwa mfano bora.

Ramadhani Brothers wameshinda tuzo hiyo baada ya kubaki fainali na kundi la Pac na wao kuibuka mabingwa ambapo wamekabidhiwa kombe la mashindano hayo na kitika hicho cha fedha.

Wameshinida tuzo hiyo katika mashindano hayo yaliyowashirikisha mabingwa mbalimbali waliowahi kuonyesha vipaji vyao katika shindano hilo la AGT.

Serikali kupitia Mkurugenzi Mkuu Wizara wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Gerson msigwa amesema wanawatafuta vijana hao ili wafahamu wanarudi lini waweze kuandaa namna ya kuwapokea na kuwapongeza.

Ramadhani Brothers waliwahi kushiriki mashindano mbalimbali ya vipaji kwa nchi mbalimbali lakini hawakufanikiwa kushinda lakini Rais Samia Suluhu Hassan aliwapongeza kwa juhudi walizozionyesha pamoja na kuitangaza nchini.

Habari Zifananazo

Back to top button