‘Siku ya kufyeka vichaka imefika’

Wachezaji wa kikosi cha Yanga wakifanya mazoeizi hivi karibuni.

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika(CAF) hatua ya awali, Yanga leo inashuka dimba la New Amaan Complex, Zanzibar katika mchezo wa marudiano dhidi ya CBE SA ya Ethiopia.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Septemba 14 kwenye uwanja wa Abebe Bikila uliopo mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, Yanga ilishinda kwa bao 1-0 likifungwa na Prince Dube.

SOMA: “Yanga tunataka kuongoza kundi”

Advertisement

Akizungumza Septemba 20 Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kikosi kipo katika hali nzuri na wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano.

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi.

“Nina wachezaji wakubwa sana ambao wanaweza kufanya jambo bora kuliko wapinzani wetu, najua wachezaji wangu wanafahamu umuhimu wa kufuzu hatua ya makundi,” amesema Gamondi.

Michezo mingine ya kufuzu makundi Ligi ya Mabingwa Afrika leo ni kama ifuatavyo:

TP Mazembe vs Red Arrows
Petro Atletico vs Maniema Union
Al Ahly vs Gor Mahia
Mamelodi Sundowns vs Mbabane Swallows
Orlando Pirates vs Galaxy
Esperance vs Dekedaha
Pyramids vs APR
MC Alger vs US Monastir
Raja Casablanca vs Samartex