Someni vitabu muongeze maarifa

UTAMADUNI wa kusoma vitabu nchini umeendelea kupungua hali inayozua mjadala kuhusu umuhimu wa vitabu katika kuongeza maarifa na kujenga uwezo wa jamii kuanzia ngazi ya familia  hadi Taifa.

Mwandishi wa vitabu, Hamisi Kibari, amesema kuna haja ya jamii kurejea katika utamaduni wa kusoma vitabu kwa kuwa ni chanzo muhimu cha maarifa na uelewa wa masuala mbalimbali.“Vitabu vina maarifa kwani kabla ya kuandika kitu mwandishi huwa amefanya utafiti. Kupitia vitabu, mtu anaweza kufahamu mambo mengi na pia kujifunza lugha kwa ufasaha,” amesema.

Kibari amesema wazazi wana nafasi kubwa katika kujenga utamaduni wa kusoma kwa watoto lakini baadhi yao hawana utaratibu wa kusoma vitabu au kuwahamasisha watoto kusoma kazi mbalimbali za fasihi, ikiwemo riwaya na tamthilia. Amesema jamii inapaswa kubadilika na kurejea katika usomaji wa vitabu kwa kuwa husaidia kuongeza maarifa na kujenga  uwezo wa kufikiri na kuelewa masuala yanayoizunguka.

Kwa upande wake, mfanyabiashara wa vitabu, Michael Mtundu, amesema Watanzania bado wanasoma vitabu ingawa idadi yao si kubwa huku baadhi wanatumia mitandao kusoma kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. “Kwa sasa Watanzania wanasoma vitabu kwa sababu wanakuja kununua kwetu, lakini idadi si kubwa sana. Wengine pia wanasoma kwa njia ya mtandao,” amesema.

Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wamesema wana mwamko mdogo wa kusoma vitabu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa muda. Mkazi wa Dar es Salaam, Paschal Msengi, amesema mara nyingi husoma vitabu vya kiada anapokuwa na lengo maalumu, hasa anapopewa kazi chuoni. SOMA: Watoto wafundishwe kusoma vitabu

“Huwa nasoma vitabu vya kiada nikiwa na lengo la kutafuta jambo fulani, hasa baada ya kupewa kazi chuoni, ila vitabu vingine sisomi kutokana na muda,” amesema. Hadi sasa Takwimu za Kitaifa za usomaji wa vitabu 2023 zinaonyesha kuwa asilimia 59% ndio wanasoma vitabu na uwezo wa kusoma vitabu kwa Tanzania inafikia asilimia 76% mwaka 2020/21.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button