SUA yachangia tafiti udhibiti magonjwa

MOROGORO: CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),kupitia Ndaki ya Tiba ya Wanyama na Sayansi za Afya kimeendelea kutoa watafiti bora na bobezi wanaofanya mambo makubwa katika kulisaidia taifa na nchi nyingine barani Afrika kwenye kudhibiti magonjwa ya wanyama na yale yatokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
Rasi wa Ndaki ya Tiba ya Wanyama na Sayansi za Afya ,Profesa Esron Karimuribo amesema hayo akielezea hatua mbalimbali tangu mwaka 1976 ilipoanzishwa sehemu ya wanyama chini Kitivo cha Kilimo Misitu na Sayansi za Afya eneo la Morogoro kikiwa chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Profesa Karimuribo amesema kuwa baadhi ya watafiti wametangulia mbele ya haki , Mungu amewaita akiwemo Profesa Rudovick Kazwala aliyekuwa mhadhiri na mtafiti nguli wa Ecosystems na Afya ya Umma ya Wanyama na alitambuliwa mwanasayansi nambari moja nchini Tanzania mwaka 2021.
Amesema mchango mkubwa uliofanywa na ndaki hiyo ni utafiti wa kuthibiti ugonjwa wa kifua kikuu kinaenezwa na wanyama kutokana na kunywa maziwa ambayo hayajachemshwa vizuri ndani yake kuna wadudu wanaosababisha kifua kikuu kinachokuwa nje ya mfumo wa upumuaji.

‘ Kwa muda mrefu watu wa sekta ya afya alidhani kuwa kifua kikuu kinaenezwa tu kwa njia ya hew ana katika sehemu hii tumefanya vizuri” amesema Profesa Karimuribo.
Profesa Karimuribo amesema kupitia Ndaki hiyo Chuo Kikuu imewezesha kusaidia utafiti wa kudhibiti magonjwa ya mlipuko na moja ya rekondi nzuri ni m waka 2020/2021 baada ya kutokea kwa ugonjwa wa Covid -19 .
Amesema kwa kuwa ugonjwa huo ulikuwa mpya na ulijitokeza ghafla ,Chuo Kikuu kupitia Ndaki hiyo kilikuwa ni kitovu cha watafiti wabobezi ambao walisaidia Maabara ya Taifa kufanya utambuzi wa kwanza wa mama mmoja aliyeingia na ugonjwa huo kutoka nchi za Ulaya.
Profesa Karimuribo amesema kupitia ndaki hiyo imeezesha pia kuwepo mifumo na teknolojia kwa kubuni mfumo unaojulikana Afya ya Msafiri unaorahisisha utendaji kazi maeneo ya viwanja vya ndege kwa utambuzi wa vihatarishi wa magonjwa ya kuambukiza.

Amesema mafanikio mengine nje ya mipaka , ni baada ya timu maalumu watafiti iliyo kusaidia kudhibiti ugonjwa wa Covid -19 katika nchi jirani inayopakana na Tanzania baada ya kuombwa.
Profesa Karimuribo amesema mwaka 2023 walipata ombi kutoka Guinea , Conakry ipatiwe wataalamu ambapo “yeye” aliongoza kikosi kazi kwenda kuboresha mifumo yao ya kufuatilia magonjwa ya Wanyama kupitia app ya afya data na kuweka katika nchi hiyo na inafanya kazi vizuri.

Amesema Ndaki inapata wanafunzi wengi kutoka mataifa mbalimbali yakiwemo ya Lethoto , Namibia , Madagascar , Burundi , Rwanda , Kenya , Uganda , Sudani na Nchi za Afrika Magharibi zikiwemo za Nigeria , Bukinafaso na Ivory Coast
Kwa upande wake mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Ndaki hiyo, Anna Boma amewaomba wazazi na jamii iwape fursa watoto wakike kusoma masomo ya sayansi shule za sekondari ili yawe ni daraja kujiunga na e limu ya juu , na baadaye waje kuwa wanataaluma bora.



C168 mang đến hệ sinh thái giải trí trực tuyến gồm casino, cá cược thể thao, bắn cá, nổ hũ, game bài và xổ số, giao diện hiện đại, thao tác thuận tiện trên nhiều thiết bị.
I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
This is what I do….. https://www.work27.info
I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
This is what I do….. https://www.work27.info