Tandahima yarejesha makato ya Sh 20 kilo ya korosho

MTWARA: BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, limedhamiria kurudisha tena makato ya Sh 20 kwa kila kilo moja ya zao la korosho kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye halmashauri hiyo.
Hayo yamejiri wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Tandahimba kuhusu utekelezaji wa taarifa za kata robo ya nne mwaka wa fedha 2025/2026 kilichofanyika katika Wilaya ya Tandahimba mkoani humo.
Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Azizi Selemani, amesema Tandahimba ni miongoni mwa wilaya zinazozalisha kwa wingi zao la korosho ambalo limekuwa likichangia maendeleo katika ngazi ya halmashauri na vijiji.

“Kutokana na hali hiyo tumeona ni vyema kurejesha makato ya Sh 20 kwa kila kilo moja ya korosho ambayo hapo awali wakulima walikuwa wakichangia kwa ajili ya maendeleo,”amesema Selemani
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Michael Mtenjele amesema maelekezo yalishatolewa ya kutaka wakulima kufanya mikutano kwenye vijiji na kupitia vyama vyao vya ushirika ili wakubaliane kwa hiari kuhusu makato hayo.

“Kuhusiana na Sh 20 maelekezo yalishatolewa kwamba vijiji vyetu vikae kwenye mikutano yao na vyama vyao vya ushirika wakubaliane kwamba sisi tumeridhia, waandike barua kuthibitisha kwamba wameridhia kukatwa”amesema Mntenjele
Ameongeza: “Ili kusije kuwa na mkanganyiko wa wengine kusema hawataki wengine wanataka kwa sababu hiyo ni hela yao hivyo ridhaa itoke kwenye kila kijiji na kila AMCOS”
Kutokana na hilo, mwenyekiti huyo wa halmashauri amewaomba atendaji wa kata kuandaa mikutano kwa ajili ya kuwaeleza wananchi kuhusu makato hayo ya Sh 20 lakini pia faida zinazopatikana kupitia fedha hizo.

Baadhi ya madiwani wa kikao hicho akiwemo Diwani wa Kata ya kwanyama, Hamza Salumu ameunga mkono hoja hiyo na kwamba fedha hizo zimekuwa zikisaidia kutekeleza kazi mbalimbali za maendeleo, ikiwemo kukamilisha baadhi ya miradi ambayo haijakamilika.




I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
This is what I do….. https://www.work27.info
I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
This is what I do….. https://www.work27.info