Tanzania U12 wasichana kutwaa kombe China leo?
TIMU ya Taifa ya wasichana chini ya miaka 12 itashuka dambani leo mchana kwa saa za Tanzania kukiwasha dhidi ya Sporting Lisbon ya Ureno katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mashindano ya Female Universal Youth yanayofanyika China.
Tanzania U12 imetinga fainali baada ya kuichakaza Mongolia katika mchezo wa nusu fainali kwa mabao 7-0 kwenye uwanja wa kituo cha Dingnan Youth Football.
Timu hiyo ya Tanzania U12 inanolewa na kocha Elieneza Nsanganzetu.
Kufika fainali Tanzania U12 imecheza michezo 5 ikishinda yote, kufunga jumla ya mabao 30 na haijafungwa bao lolote.
SOMA: Tanzania U12 wasichana yafanya mauaji China
Mtiririko wa ushindi Tanzania michezo iliyopita ikianza ya hivi karibuni ni kama ifuatavyo:
Tanzania U12 7-0 Mongolia
Tanzania U12 2-0 Dingnan
Tanzania U12 5-0 Shantou FA
Tanzania U12 10-0 Dream City
Tanzania U12 6-0 Indonesia