Ufadhili watikisa mapambano ya VVU

WAKATI Tanzania ikiendelea kupata mafanikio katika mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI (UNAIDS) limeonya kuwa kupungua kwa ufadhili wa kimataifa kunaweza kuhatarisha mafanikio hayo.

Takwimu za Utafiti wa Kitaifa wa Athari za Virusi vya Ukimwi Tanzania 2022/2023, uliofanywa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kwa kushirikiana na Serikali, zinaonyesha kuwa watu wazima wapatao milioni 1.55 wanaishi na VVU nchini, huku kiwango cha maambukizi kikiwa asilimia 4.4.Utafiti huo pia unaonyesha kuwa Tanzania inarekodi wastani wa maambukizi mapya 60,000 ya VVU kila mwaka miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 15 na kuendelea.

SOMA: Serikali yaongeza kasi mapambano dhidi ya Ukimwi

Aidha, matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa asilimia 82.7 ya watu wanaoishi na VVU wanajua hali zao, asilimia 97.9 ya wanaojua hali zao wanatumia dawa za kufubaza virusi (ARV) huku asilimia 94.3 ya wanaotumia dawa hizo wakiwa wamefikia kiwango cha kudhibiti virusi mwilini, hatua inayoonyesha maendeleo katika utoaji wa huduma za matibabu na ufuatiliaji.

Hata hivyo, ripoti mpya ya UNAIDS iliyozinduliwa Rio de Janeiro, Brazil, imeonya kuwa dunia imeingia katika kipindi cha ubanaji wa matumizi na kupungua kwa ufadhili wa sekta ya afya hali inayoweza kuathiri upatikanaji wa huduma za kinga, upimaji na matibabu ya VVU katika nchi nyingi, ikiwemo Tanzania.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ufadhili wa kimataifa wa mapambano dhidi ya UKIMWI ulipungua kwa asilimia 18 mwaka 2025 na kufikia dola bilioni 7.3, kiwango cha chini zaidi katika kipindi cha karibu miongo miwili. Kabla ya kuingia madarakani kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, Marekani ilikuwa mfadhili mkuu wa mapambano dhidi ya UKIMWI duniani, ikichangia takribani asilimia 75 ya ufadhili wote wa kimataifa.

Wataalamu wa afya wanaonya kuwa endapo pengo la ufadhili halitazibwa, baadhi ya nchi zinazotegemea misaada ya nje kugharamia huduma za kinga, upimaji na matibabu ya VVU zinaweza kushuhudia kuongezeka kwa maambukizi mapya na kudorora kwa mafanikio yaliyopatikana katika miaka ya karibuni.

Kwa Tanzania, tahadhari hiyo inaibua umuhimu wa kuendelea kuimarisha vyanzo vya ndani vya ufadhili wa mapambano dhidi ya VVU ili kuhakikisha huduma za kinga, upimaji na matibabu zinaendelea kutolewa bila kutetereka hata kama misaada kutoka kwa wahisani wa kimataifa itapungua.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..    https://www.work27.info

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button