Ujenzi wa madarasa Sekondari Segese wazidi kuimarisha elimu

SHINYANGA: Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang’onda, ameipongeza Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Segese iliyopo kijiji cha Busungo kwa gharama ya zaidi ya Sh milioni 45.5.

Mwang’onda ametoa pongezi hizo leo alipokuwa akiweka jiwe la msingi kwenye vyumba vya madarasa hayo ambavyo vinatarajia kukamilila mwezi Septemba mwaka huu.

Mwang’onda amesema halmashauri hii imeanza kazi ya maandalizi kwaajili ya kupokea wanafunzi mwaka 2028 amvapo elimu imekuwa ya lazima kwa mtoto kusoma miaka kumi

“Nipo tayari kuweka jiwe la msingi na vyumba vimejengwa vizuri kwa kiwango kwani hivi sasa elimu ni lazima kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne hivyo serikali ya awamu ya sita inataka watoto wote wasome,”amesema Mwang’onda.

Mkuu wa shule hiyo, John Marry akitoa taarifa kwa kiongozi huyo amesema shule hiyo ina wanafunzi 144 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne huku akieleza mradi umetekelezwa kwa force akaunt na wazabuni wa vifaa walipatikana kupitia mfumo wa manunuzi ya Umma (NeST).

Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mabula Magangila amesema kuna shule za msingi 125 na sekondari 29 na mpango mkakati kila kijiji kuwe na shule ili watoto wasitembee umbali mrefu kutafuta elimu.
mwidho

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button