VETA yapongezwa teknolojia bunifu

DODOMA: KATIBU Tawala wa Mkoa wa Singida, Dk Fatuma Mganga, ameipongeza Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa kubuni teknolojia na bidhaa zinazolenga kuongeza tija kwa wakulima na wafugaji nchini.
Dk Mganga ametoa pongezi hizo leo Agosti 4, 2026 alipotembelea banda la
VETA kwenye Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Kitaifa (Nanenane), katika viwanja vya Dk John Malecela, Nzuguni jijini Dodoma
.
“Tumeona jinsi VETA wanavyojitahidi kutengeneza mashine mbalimbali ambazo zinarahisisha kazi kwa wakulima na wafugaji katika maeneo yetu. Tumeona mashine mbalimbali zinazowafaa wakulima na wafugaji kama ile ya kuchanganyia chakula cha mifugo, mashine kama hizi zinaweza kusaidia sana wananchi,” amesema Dk. Mganga.
Dk Fatuma ameongeza utumiaji wa mashine rahisi kama alizoziona VETA zitasaidia kuongeza tija na faida zaidi katika uzalishaji.
“Niendelee kuwapongeza ndugu zetu wa VETA, naomba waendelee kushirikiana na wahitaji ambao ndiyo soko, ili tuweze kuendelea kusukuma etekeleazji wa Dira 2050 ninaamini kwa hizi teknolojia wametuonesha lengo la Dira tutalifikia hata kabla ya 2050 kwasababu wanachi wengi watawezeshwa kwa mitaji iliyopo na mitambo inayotengenezwa na wabunifu kutoka veta,” ameongeza.
DkMganga ameiomba VETA kushirikiana na ofisi za mikoa, wilaya na halmashauri ili kuweza kukutanishwa na watumiaji wa bidhaa na ubunifu mbalimbali, kwani wapo vijana kupitia vikundi wanapatiwa pesa kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali ambao wanahitaji vifaa na mashine kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.



