Wadau wapatiwa mafunzo uthibiti ubora wa elimu Mwanza

MWANZA: TAKRIBANI wadau wa elimu 200 wamepatiwa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kidigitali wa uthibiti ubora wa elimu mkoani Mwanza, wakasema matarajio yao ni kuleta kasi ya uwazi na uwajibikaji katika sekta ya elimu.

Matarajio mengine ni kupunguza matumizi ya karatasi, hatua itakayochochea utunzaji wa mazingira pia, wamesema washiriki wa mafunzo hayo kutoka mikoa yote ya Kanda ya ziwa, Tabora na Kigoma, wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo

Mhadhiri katika Taasisi ya Teknolojia Dar Es salaam, Joseph Matiko, ambaye alikuwa mshauri elekezi katika usanifu wa mfumo huo amesema uwajibikaji na uwazi utatokana na ukweli kwamba taarifa zote muhimu zitakuwa zikipatikana kwa wakati na kuonekana kwa wadau wote, kwa sababu mifumo ya taasisi mbalimbali ya serikali sasa inasomana.

“Hata jamii itakuwa na uwezo wa kupata taarifa za mfumo huo, ili kutambua ubora wa taasisi zetu za elimu,” amesema.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Carolyne Nombo, amesema pamoja na mambo mengine, mfumo huo utapunguza gharama za watumishi kwenda vijijini kukusanya taarifa za udhibiti ubora wa elimu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button