Watu 179 wafa ajali ya ndege Korea Kusini

KOREA KUSINI: WATU 179 wamekufa baada ya ndege kuanguka wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa Muan nchini Korea Kusini. Taarifa ya mtandao wa NBC News inaeleza huenda vifo vikaongezeka zaidi, kwani awali ilikuwa 149.

Ndege hiyo Boeing 737-800 ilibeba abiria 181 ilianguka uwanjani hapo ikitokea Bangkok nchini Thailand. Watu wawili walinusurika kufa na kuokolewa wakiwa na majeraha.

Kwa mujibu wa CNN, saa moja iliyopita idadi ya vifo ilikuwa 149, kati ya hao, 71 ni wanaume na 69 ni wanawake, baadhi yao tisa hawakutambuliwa jinsia kwani miili iliharibiwa vibaya.

Advertisement