DC Kilosa afanya ziara kusikiliza kero, kutatua migogoro

MOROGORO; Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka, akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama Wilaya, amefanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi Tarafa ya Mikumi na kutatua kutatua migogoro.

Pia katika ziara hiyo amekagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Kijiji cha Nyamfisi na kufanya mikutano ya hadhara kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo katika Kata za Vidunda, Ruhembe, Kidodi na Ruaha.




