Kafulila apongezwa mihadhara yenye tafiti za kina

DAR ES SALAAM: Mhadhiri wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) Jackson Muhoho, ameitaja mihadhara inayotolewa vyuoni na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia (PPPC), David Kafulila kuwa ni ya viwango, iliyo na tafiti za kina, na uwasilishaji wake ni wa kisayansi.

Mhadhiri huyo wa masuala ya mipango na mikakati amesema kuwa, mihadhara ya kisomi kwenye masuala ya utawala na uchumi hupimwa kwa misingi mitano: mifumo ya utawala, uchambuzi wa sera, mifumo ya kitaasisi, hitoria na tathmini na ufuatiliaji. Kwa maoni yake anasema kuwa, mihadhara ya Kafulila inatimiza vigezo hivyo.

Ni kwa misingi hiyo, Muhoho anashauri mihadhara ya aina hii kuwekewa utaratibu ambao unaweza kuwa sehemu ya mchango wa kisera katika mifumo ya uchumi wa Tanzania.
Wakitoa maoni kuhusu mtazamo wa Muhoho, wahadhiri na wanafunzi walioshiriki mhadhara huo walikubaliana na hoja hii.



