Visima kuongeza upatikanaji maji Nyang’hwale

GEITA: WAKALA wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imesema Mradi wa Maji wa Visima 5 vya Jimbo wilayani Nyang’hwale mkoani Geita umeongeza upatikanaji wa maji kutoka asilimia 77.4 hadi asilimia 79.6

Meneja wa RUWASA wilayani Nyang’hwale, Mhanidisi Suzana Mabula ametoa taarifa hiyo mbele ya viongozi wa mbio za Mwenge kitaifa kwa mwaka 2026 katika kata ya Kanegele wilyani humo.

Amesema mradi huo umetekelezwa katika Vijiji vya Kanegele, Mwingiro, Shabaka, Wavu na Lubando na unazalisha jumla ya lita 21,150 kwa saa ambapo takribani wananchi 5,000 ambapo watapata huduma ya maji safi na salama.

“Mkataba wa Ujenzi wa Vioski ulianza rasmi mnamo Julai 01/2025 na ulitarajiwa kukamilika Septemba 02, 2026 lakini hadi kufika Agosti 10, 2026 mradi ulikuwa tayari umekamilika”, amesema Suzana.

Suzana amesema gharama za utekelezaji wa Mradi wa Maji katika Vijiji hivi vitano (5) ni sh milioni 336 na hadi sasa Jumla ya kiasi cha sh milioni 245 kimekwisha kutumika.

“Chanzo cha fedha za Mradi huu ni kupitia Mpango wa Malipo kulingana na Matokeo (PforR) na Fedha Maalum (Special Fund)”, amesema Mhandisi Suzana.

Ametaja miongoni mwa shughuli zilizofanyika ununuzi wa matenki ya plastiki yenye ujazo wa lita 10,000 na kulaza mabomba na kufukia umbali wa mita 9,467, Ujenzi wa chemba kubwa tano na ndogo sita za maji.

“Uendeshaji wa mradi huu upo chini ya Jumuiya ya Watoa Huduma ya Maji ngazi ya Jamii(CBWSO’s) ya Nyamtukuza visima Vitatu na JWPP visima Viwili”, amesema Suzana.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mwaka 2026, Wazo Michael Mwang’oda amezindua mradi huo na kusisitiza kuwa dhamira ya serikali na kuhakikisha wananchi wake wnaapata maji safi na salama hivo usimamizi thabiti wa mradi huo ufanyike.

Amesema wilaya ya Nyang’hwale ni miongoni mwa maeneo ambayo serikali inaendeelea kuwekeza ujenzi wa mbalimbali kwa maslahi ya jamii na hivo viongozi wanapaswa kusimamia kikamirifu ili malengo ya utatuzi wa changamoto za kijami yafikiwe.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button