CCM yamfuta uanachama Balozi Nchimbi

DAR ES SALAAM – Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemfuta uanachama aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.
Uamuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro, katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi ndogo za CCM, Lumumba, Dar es Salaam.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Nchimbi kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais, akisema ameamua kustaafu siasa na utumishi wa umma kuanzia Septemba 4, 2026. Rais Samia Suluhu Hassan aliridhia ombi hilo.
Katika hatua nyingine, CCM imempendekeza Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, kuwa Makamu wa Rais mpya, pendekezo linalofuata kujiuzulu kwa Nchimbi.



