‘Serikali imeanza mchakato ujenzi wa meli mpya’

MTWARA; NAIBU Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema serikali imeanza mchakato wa ujenzi wa meli mpya ya mizigo katika Bandari ya Mtwara, itakayosaidia kuboresha huduma za usafirishaji majini, Kanda ya Kusini.

“Kwa sasa serikali ipo kwenye hatua ya kumtafuta mzabuni wa mradi huo wa ujenzi wa meli, ” amesema na kuongeza kuwa mchakato wa kumtafuta mzabuni utakamilika mwezi Desemba 2026 na ujenzi wake kuanza.

Kihenzile ameeleza hayo leo Septemba 9, 2026 kwa wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, waliofika Mtwara kukagua miradi ya maendeleo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Seleman Kakoso amepongeza serikali kwa hatua hiyo ya ujenzi wa meli huku akitaka wizara ya Uchukuzi kuharakisha ujenzi wa barabara ya kutoka Dar kwenda Mtwara kwa lengo la kuboresha zaidi usafiri.

Amesema barabara ya kutoka Dar es Salaam kwenda Mtwara ni mbaya akisisitiza ujenzi wake ujengwe na kuboreshwa haraka.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wametembelea na kukagua ujenzi wa Bandari ya Mizigo Mikubwa ya Kisiwa Mgao, Halmashauri ya Mtwara na Bandari Mama Mtwara mjini.

Wajumbe hao wamepongeza serikali kwa ujenzi wa mradi wa Bandari mpya ya Kisiwa Mgao, huku wakitaka ujenzi uharakishwe kuruhusu huduma za kusafirishaji katika Bandari hiyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button