Watumishi Nanyamba watakiwa kusikiliza wananchi

MTWARA; WATUMISHI wa serikali kwenye Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwar, wametakiwa kuwasikiliza wananchi waliopo kwenye maeneo yao, ili kuwezesha maendeleo ya wananchi.
Hayo yamejiri leo Septemba 9,2026 wakati wa ziara ya kikazi iliyofanywa na Mbunge wa Jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota kwenye Kata ya Njengwa.
Mbunge huyo pia alisikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hao na kuzifanyia kazi kama vile ujenzi wa ofisi ya Kijiji cha Mtendachi pamoja na Mhule ya Msingi Mtendachi juu ambayo iko hatua ya linta. Mbunge huyo ametoa msaada wa mifuko 50 ya saruji itakayosaidia kwenye miradi hiyo.
Mbunge Chikota amewasisitiza wananchi hao wajenge uhusiano mazuri baina yao na watumishi hao ili kuharakisha maendeleo.
Akizungumzia suala hilo la watumishi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mtwara Vijijini, Nashir Mfaume amesema serikali iliyopo madarakani ni ya CCM, lakini Ilani inayotekekezwa ni ya chama hicho.

Amesema watumishi hao wanatekekeza Ilani hiyo na Rais Samia Suluhu Hassan anatamani kuona wananchi wanahudumiwa na kusikilizwa.
“Wapo baadhi ya watumishi wamekuwa changamoto, kwa hiyo niwaombe tuwasikilize wananchi wanapokuja kwetu na tuwape majibu ya changamoto zao, yale ambayo yako ndani ya uwezo wako yachukue na yaliyopo juu yako yabebe,”amesisitiza Nashir na kuongeza:

“Kwa sababu leo miradi ikijengwa hapa kesho mtendaji amehama hiyo miradi itabakia hapa kwa hiyo unapomsusia kushiriki shughuli za maendeleo maana yake tunajikwamisha sisi wenyewe wananchi kupata maendeleo.”



