Mradi wa mfano usafi wa mazingira wafikia asilimia 88

DAR ES SALAAM; Mradi wa kwanza wa kisasa na usafi wa Mazingira Afrika Mashariki wa kuchakata majitaka umefikia asilimia 88 ya utekelezaji wake, huku ukitajwa kunufaisha kaya takribani 11,000 Wilaya ya Kinondoni.
Mradi huo uliopo eneo la Mbezi Beach unatekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) na utagharimu kiasi cha Sh bilioni 124 ukikamilika.

“Mradi unahusisha, ulazaji wa mtandao wa bomba za majitaka kilometa 101, ujenzi wa vituo viwili vya kusukuma majitaka, ujenzi wa chemba zaidi ya 2,300 pamoja na ujenzi wa mtambo wa kisasa wa uchakataji majitaka,” imesema taarifa ya Dawasa kwa vyombo vya habari na kuongeza:

“Mradi huu unategemea kukamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba,2026 utanufaisha zaidi ya kaya 11,000 katika kata nne za Kawe, Kunduchi, Mbezi Juu na Wazo wilayani Kinondoni, huku ukitegemewa kutoa bidhaa nyingine muhimu kama vile mbolea na gesi.”



