Ukatili unavyowakumba watoto wanaokimbia familia na kuishi mtaani

“NILIPOKIMBIA nyumbani nikaenda kuishi mtaani na baadae nikaja Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kutafuta maisha mazuri zaidi ,lakini nilivyoingia nilikutana na ukatili wa kila aina mkubwa zaidi ni kulawitiwa na wakubwa hi indo inaniuma sana ,”anasimulia Benjamini(12) ambalo sio jina lake halisi.

Anasema kilichomtoa nyumbani kwako Morogoro ni baada ya kukutana na mateso makali kutoka kwa shangazi yake aliyekuwa anamlea baada ya wazazi wake kutengana na kila mmoja kuhamia mkoa mwingine sehemu asipopajua yeye.

“Nilishindwa kuvumilia vipigo na kunyiwa chakula mateso yalikuwa mengi sana nikaamue niende kutafuta sehemu salama ya kuishi lakini huku nilipo kuna mateso na ukatili wa kila aina siku waliponiona mgeni kuna mkubwa aliniingili kwa nguvu sikuwa na la kufanya wala pa kushtaki nilibaki ninalia kwa maumivu nikahama eneo hilo ilikuwa Ubungo nikaenda Mwenge pale mataa,”anaeleza.

Benjamini ni miongoni wa watoto wengi walioko mtaania ambao wanakabiliwa na ukatili na hatari kubwa sana.Kwa Mujibu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa idadi kubwa ya watoto wanaoishi mitaani na kufanya kazi baada ya kukimbilia familia zao kutokana na migogoro ya ndoa.

Mikoa inayofuatia kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto hao  ni Mwanza, Dodoma, Mbeya Arusha na Iringa.Aidha mikoa inayochangia watoto hao kukimbia familia zao na kuiingia mjini ni Kagera, Geita, Kigoma, Dodoma, Mwanza na Shinyanga.

Takwimu za wizara hiyo zinaonesha kuwa katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025, watoto 8,372 wa aina hiyo waliokolewa na kuwezeshwa kwa kupatiwa huduma mbalimbali.Kati ya watoto hao, 1,056 wanahifadhiwa nyumba salama, 86 kwa walezi wa kuaminiwa na waliosalia  wanaishi na familia zao.

Zaidi ya watoto  1,346 kati ya waliokolewa, walipatiwa vifaa vya shule na mahitaji mengine, 43 walipelekwa vyuo vya ufundi, 27 wamehitimu na wawili kufanya kazi za kujitolea katika makazi ya wazee.Kati ya Julai hadi Desemba 2024, manusuru 27,479 walipatikana,  kati ya hao  watoto 50,040  na watu wazima 12,439 walipatiwa huduma katika madawati ya jinsia na watoto.

Hata hivyo utafiti umebaini kuwapo kwa migogoro ya ndoa  16,095 nchini, ambayo baadhi imechangia watoto hao kukimbilia mitaani na kuishi katika mazingira magumu na kufanya kazi ili wapate kipato cha kujikimu na maisha. Wizari inasema migogoro hiyo  imeshughulikiwa kupitia ofisi za ustawi wa jamii nchini kwa kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025 hatua itakayopunguza wingi wa watoto kuingia mitaani.

AISHI MTAANI KWA MIAKA 23

James Yusta ni kijana ambaye ameishi mtaani kwa takribani miaka 23 baada ya kukimbilia mtaani akiwa na umri wa miaka saba alivyonusurika kuuawa na mjoba yake isili asirithi mali ya marehemu mama yake.

James ambaye ni mzaliwa wa jiji la Arusha alilelewa na mtawa wa kanisa Katoliki baada ya mama yake mzazi kumtupa katika jalala haifahamiki ni kwanini hata leo.Akiwa mtaani kwa wakati huo alipitia mateso mengi ambayo badala ya kumvunja moyo alizidi kujipa matumaini ikiwemo kipigo,kunusuruka kulawitiwa,kunywang’anywa vitu,kunyeshewa na mvua na adha zingine.

“Nilikuwa bado na malengo ya kufanikiwa hivyo nilijiepusha na matumizi ya dawa za kulevya  huku nikijituma kufanya kazi kwa bidii na hatimaye nikafanikiwa kupata fedha ya kupanga chumba ila haikuwa rahisi.Baada ya siku kusonga anasema alifanikiwa kupata kazi nzuri huku akiendelea kupigania ndoto za kuanzisha taasisi ya kuwasaidia watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.

“Namshukuru Mungu bila yeye nisingefika hapa nilipo leo nina taasisi yangu inaitwa James Foundation inasadia hawa watoto na tayari nimesharusdisha watoto 150 kwa familia zao nah ii ni kutokana na kujua mateso makala wanayipata watoto hao mitaani,”Anasisiza James.

Miongoni mwa vitu ambavyo alivitaja kuwa ni maumivu yasiyosahaulika kwa watoto wa mitaani ni ya mtoto anayeitwa Rashid mwenye umri wa miaka 11 kutoka singida . “Mtoto huyu alikuwa anaingiliwa kinyume na maumbile na baba yake wa kambo lakini alipomwambia mama yake kuwa baba anamfanyia kitendo hicho mama yake hakumsaidia bali alimchapa na baada ya mtoto kuona hapati msaada wowote akakimbilia mtaani Singida .

“Baada ya miezi mitatu akaja Dar es Salaam  na nilipokutana naye nilimuuliza na nikataka kumrudisha kwao lakini alikataa kurudishwa. Anasema baada ya kumdadisi sana kwanini hataki kurudi akamweleza mkasa wa baba yake wa kambo nikampeleka hospitali ya Palestina .

“Nilivyofika Hospitali ya Palestina wakanipa rufaa kwenda Hospitali ya Mwananyamala huko ndio anatapata uchunguzi na matibabu zaidi na hapo kuna dirisha la sheria .Nilivyoenda kweli nilikuta maafisa ustawi tukaungana mtoto akapimwa na kweli vipimo vilionesha anaingiliwa kinyume maumbile . Anabainisha kuwa baada ya hayo walifungua kesi na kuifuatilia lakini cha kusikitisha mtoto rashidi alikuja kufariki kwa kugongwa na gari.

“Hiyo iliniumiza sana kwasababu misukosuko imefanya maisha yake kupotea mapema.Baada ya kuwafuatilia ndugu zake hawakutokea hivyo alizikwa na Manispaa hata hivyo baada ya kusambaza picha kwenye mitandao ndugu zake wakajitokeza  wakaja Dar es Salaam nikawaonesha kaburi.

KINACHOWAFANYA WAKIMBILIE MITAANI

Kwa mujibu wa James watoto wengi wanaokimbia mtaani anaowahoji walisema wanakimbia vipigo na kunyimwa chakula kutoka kwa wazazi au walezi wao .“Wakiniambia ni kipigo nawafikiri kwa pande mbili huenda mtoto ni mtukutu hata kusiki anachofundishwa au ananyanyaswa na ninafatilia tabia ya kila mmoja halafu nawashauri na kuwafundisha jinsi ya kuishi na wazazi

“Wengi wao wanakubali kurudi nyumbani na kubadilika na nimefanikiwa kuwarudisha watoto 150 kwa wazazi wao katika mikoa ya Mbeya,Mwanza,Arusha,Dodoma ,Iringa ,Kilimanjaro na Mikoa mingine.SOMA: Tabora yadhibiti watoto wa mitaani

James Anasimulia habari ya mtoto aliyekimbia kwa wazazi kutokana na adhabu kali “Alitumwa dukani na mama yake akanunue mchele kwa bahati mbaya alijikwaa akamwaga hivyo hakuridi tena nyumbani .“Aliwahi kushudia dada yake akichomwa moto na mama mzazi baada ya kumwaga unga kwa bahati mbaya hivyo kwa kuogopa akaenda kuishi mtaani ,alikuja Dar baada ya siku tatu nilikutana naye akanieleza huo mkasa ikabidi maafisa ustawi wamtafute mama na baada ya kuzungumza naye mtoto alirudishwa shuleni

MAISHA YA MTAANI NI MAUMIVU

James anasimulia kuwa alianza kukaa mtaani akiwa na umri wa miaka saba na kuishi mtaani kwa miaka 23  baada ya kunusurika kuwawa na mjomba wake baada ya mama yake mlezi kufariki.

“Ninajua kila kitu mtaani mtoto anapokelewa na ukatili wa kila aina kama kupigwa,kulawitiwa,kuvuliwa nguo ,kunyang’anywa vitu vyako,usiku unakuwa mchungu sana.Na kwa bahati mbaya jamii inawatazama kwa jicho hasi wengi wanafikiri ni watovu wa nidhamu hawajui kuwa watoto anakaa mitaani kwa kukosa malezi bora .

Anasema watoto wote wanafamilia na sio baba na mama pekee ni pana sana watoto wanatakiwa kulelewa na ndugu kama baba mzazi anamfanyia vitendo viovu anaenda kwa mjomba ,baba mkubwa,baba mdogo ,mama mdogo na wengine.

Anaeleza zaidi kuwa viongozi  wa dini na wa serikali wananafasi kubwa sana kuzui watoto kuishi mitaani,“Fikiri mtoto anatoka Singida anakuja hadi Dar hakuna mtu anamuuliza na wengi wanakuwa na mawazo hasi,jamii ikipewa elimu ya malezi bora watoto wanaoishi mtaani hawatakuwepo .

Anasema sasa amendika kitambu kinaitwa “Sauti ya Mtoto wa mitaani”kitabu ambacho kinapitiwa na taasisi ya elimu ili kuingia katika mifumo ya elimu kama sehemu ya mtaala kwani ameeleza shuhuda nyingi za watoto wa mitaani na jinsi ya kuwasaidia iliwema elimu ya malezi.James anapatikana kwa namba 0657579300 ikiwa unahitaji kuungana naye katika kuwasaidia watoto wanaoishi mitaani unaweza kumtafuta kwa namba hizo.

MIKAKATI  YA SERIKALI

Agosti 25 ,2025 Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dk Doroth  Gwajima alizindua mradi wa kuwasaidia watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani ijulikanano kama Children in street situation (CiSS)utakaotekelezwa katika mikoa ya Dar Es Salaam,Mwanza na Dodoma  wenye lengo la kuwapunguza,kuwapatia elimu,ujuzi na stadi mbalimbali kwa watoto waliokuwa wanaishi mitaani.

Anasema serikali imechukua msimamo thabiti  kuhakikisha hakuna mtoto anayeachwa nyuma na kwamba kila mtoto bila kujali asili,mazingira yakeanafurahia haki ya kulindwa  na kupata fursa ya kufikia uwezo wake kamili .

Anabainisha kuwa watoto wanaoishi mtaani wanawakilisha moja wapo ya makundi yaliyohatarini zaidi katika jamii kila siku wanakabiliwa na hatari zinazoweza kuathiri usalama,afya ,elimu na ustawi wao hivyo mradi huo utasaidia juhudi za serikali  kuwanusuru.

“Ninapongeza shirika la SOS Children’s Villages Internation na washirika wake  kwa maono na kujitolea kupitia mradi wa CiSS  mradi huu unaonesha jinsi uokoaji,ukarabati,urejeshaji  kwa familia na ujumuishwaji unaofanywa kwa uratibu unavyoweza kuleta matumaini mapya  kwa watoto .

Anasema serikali imefanya ulinzi kwa watoto wanaoishi mtaani kuwa kipaumbele cha taifa na wapo katika mchakato wa kuandaa mpango kazi wa kitaifa wa kumaliza changamoto ya watoto wa mitaani ambao utatumika kama mfumo kamili kwa wadau wote . Hivyo mchango wa wadau wa kitaaluma na uzoefu wa vitendo umekuwa muhimu katika kuhakikisha mpango huu unazingatia uhalisia na suluhisho za kibunifu.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to eargns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button