Familia: Hatukukaidi agizo la RC Dar

DAR ES SALAAM: Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, kuagiza wanafamilia wa David Mushi wakamatwe wakati wa ziara yake katika eneo lenye mgogoro wa ardhi lililopo Madale, Wilaya ya Kinondoni, familia hiyo imeibuka na utetezi kuwa haikuwa na taarifa kuhusu ziara hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwanasheria wa familia za Mushi na Mariam Mongi, Wilson Ogunde, Chalamila alitembelea eneo hilo Septemba 19, 2026 na kuwasikiliza baadhi ya watu waliokuwa wameondolewa eneo hilo.

Taarifa hiyo imedai baada ya ziara hiyo, Chalamila alimwagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa kuwakamata wanafamilia wa Mushi kwa kutokuwepo eneo hilo wakati wa ziara.

Familia hiyo imekanusha madai kwamba ilikaidi au kudharau mamlaka, ikisema haikupata taarifa wala wito wa kuhudhuria ziara hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, siku moja kabla ya ziara hiyo, Septemba 18, 2026, baadhi ya wanafamilia walikuwa katika kikao cha usuluhishi kilichoongozwa na Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi pamoja na wanasheria wao.

Taarifa hiyo inadai kuwa hadi saa 12 jioni, familia hizo ziliambiwa zinaweza kuondoka na zingejulishwa endapo zingehitajika, huku Kamishna Msaidizi wa Ardhi akieleza kuwa angefika eneo hilo Septemba 19, 2026.

Kwa sababu hiyo, taarifa hiyo inasema baadhi ya wanafamilia wazee walirejea Moshi, wakiwemo waliokuwa wakihitaji huduma za matibabu.

“Baada ya kupata taarifa kuhusu agizo la kukamatwa kupitia mitandao ya kijamii, wanafamilia hao walirejea Dar es Salaam na kujitokeza kwa hiari kwa mkuu wa mkoa kwa lengo la kutoa ufafanuzi na kuomba agizo hilo lisitishwe,” imedai taarifa.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa hiyo, waliamriwa kwenda Kituo cha Polisi Oysterbay na kuwekwa chini ya ulinzi. Waliokamatwa wanatajwa kuwa ni wanawake wawili wazee na vijana watatu.

Taarifa imeeleza kuwa masuala ya umiliki wa eneo hilo yamewahi kufikishwa katika Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu, ikisema maamuzi yaliyotolewa yalithibitisha haki ya Familia ya David Mushi katika eneo hilo.

Familia imewataja baadhi ya watu (majina tunayo) kwamba ni chanzo cha mgogoro huo, akiwemo kiongozi mmoja wa mtaa kwa kuhusika na ukataji wa viwanja kwenye eneo hilo au kusaini ushahidi, hivyo kuomba mamlaka husika, ikiwemo TAKUKURU na Jeshi la Polisi, kuchunguza madai yao na kuwachukulia hatua wahusika endapo itabainika walifanya makosa.

Pia wameiomba serikali kuendelea na juhudi za usuluhishi na kushughulikia kiini cha mgogoro huo, huku ikiomba Jeshi la Polisi kuzingatia haki za kikatiba za wanaoshikiliwa, ikiwemo kupata huduma za afya na kuzingatia ukomo wa muda wa kisheria wa kushikiliwa.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Home cash earning job to earns more than $220 per Hour!** getting paid weekly more than 4700+Dollar per week or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. **Want the secret?** Copy this Website and choose HOME TECH OR MEDIA…
    .
    Here is I started_____ ⫸ http://Www.Cash54.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button