Tabora yadhibiti watoto wa mitaani

ZAIDI ya watoto 20 wa mitaani katika Halmashauri ya Wilaya ya Tabora wamebainika na kupatiwa msaada kupitia juhudi za Serikali za kukabiliana na changamoto hiyo. Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Upendo Wella wakati wa ziara yake katika Kituo cha Kulea Watoto cha Igambiro alipotoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu wakiwemo yatima.

Akizungumza na Daily News Digital na Habari Leo, Wella amesema kati ya watoto hao sita wameunganishwa na vituo vinavyotoa malezi, uangalizi na huduma muhimu, huku watoto 15 wakirejeshwa kwa wazazi au walezi wao baada ya kufanyika tathmini ya mazingira yao.

Wella amesema zoezi la kuwabaini watoto wa mitaani linaendelea katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, likilenga kuwaondoa katika mazingira hatarishi na kuwapatia fursa ya kuishi maisha salama na yenye matumainiikiwemo kupata haki yao ya msingi ya elimu kama ilivyo kwa watoto wengine. SOMA: Serikali yaokoa watoto 5,353 mitaani

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button