THRDC yasisitiza maridhiano kujenga umoja

DAR ES SALAAM: MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeungana na jumuiya ya kimataifa kuadhimisha Siku ya Demokrasia Duniani, huku ukiitaka Serikali, taasisi za umma, vyama vya siasa, wananchi na wadau wengine wa demokrasia kuanzisha na kuendeleza mazungumzo na maridhiano kwa lengo la kupunguza migawanyiko, kujenga umoja na kurejesha imani ya wananchi katika taasisi na michakato ya kidemokrasia.
Wito huo umetolewa kupitia tamko la THRDC lililotolewa na kusainiwa na Mratibu wa Kitaifa wa mtandao huo, Wakili Onesmo Olengurumwa, leo Septemba 15, 2026, katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani.
Katika tamko hilo, Olengurumwa amesema demokrasia inahitaji uvumilivu wa kisiasa, huku akisisitiza kuwa kutokubaliana na Serikali, kukosoa sera au kudai uwajibikaji si uhalifu wala uadui dhidi ya taifa kwani tofauti za maoni ni sehemu muhimu ya demokrasia na zinapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria, bila vitisho, ubaguzi au matumizi yasiyo ya lazima ya nguvu. Aidha, amewataka wananchi kuheshimu maoni na uhuru wa wengine, pamoja na kukubali kutokubaliana.
“Demokrasia imara hujengwa kupitia majadiliano, ushirikiano, uvumilivu na heshima kwa mitazamo tofauti,” amesema Olengurumwa.
Akizungumzia kaulimbiu ya mwaka huu, “Deliberative Democratic Processes” (Michakato ya Kidemokrasia ya Kimajadiliano), Olengurumwa amesema kaulimbiu hiyo inasisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wananchi kutoka makundi mbalimbali katika majadiliano yenye maana ili kusaidia kuboresha maamuzi, kujenga uaminifu, kupunguza migawanyiko na kuimarisha jamii zenye amani na ushirikishwaji.
“Demokrasia haiishii kwenye sanduku la kura. Ushiriki wa wananchi unapaswa kuwepo kabla, wakati na baada ya uchaguzi, kwa kuwapa nafasi ya kushiriki katika mijadala kuhusu sera, sheria, bajeti, mipango ya maendeleo na maamuzi mengine yanayogusa maisha yao,” amesema Wakili Olengurumwa.
THRDC imeeleza kuwa demokrasia si suala la uchaguzi pekee, bali ni mchakato wa kila siku unaolenga kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa, utawala wa sheria unaimarishwa na wananchi wanashiriki kikamilifu katika maisha ya kiraia na kisiasa.
Olengurumwa amesema demokrasia ya kweli inapaswa kuzingatia kanuni kwamba hakuna mtu aliye juu ya sheria. Ameongeza kuwa mamlaka ya Serikali lazima yatekelezwe ndani ya mipaka ya Katiba na sheria, huku wananchi wakiwa na njia huru, madhubuti na zinazofikika za kupata haki pale wanapokiukwa.
Katika tamko hilo, THRDC imesisitiza umuhimu wa kuimarisha Bunge, Mahakama, taasisi za uchaguzi, vyombo vya habari, taasisi za uwajibikaji na taasisi za haki za binadamu.
“Uzoefu wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 unaongeza umuhimu wa mageuzi ya kikatiba na uchaguzi, uhuru wa taasisi, uwajibikaji wa vyombo vya dola, uhuru wa kujieleza na ulinzi wa nafasi ya kiraia,” amesema Olengurumwa.
THRDC imesisitiza kuwa kuimarisha misingi hiyo ni hatua muhimu katika kujenga demokrasia yenye ushirikishwaji, uwajibikaji, heshima kwa haki za binadamu na amani ya kudumu nchini Tanzania.




❤️ Wasichana warembo na wenye hamu ya kimapenzi kutoka kote duniani wanakungoja; jiunge hapa ………………..> https://da.gd/girls66