TFS kuwapangia vituo watumishi wapya 328

Kamishna wa Uhifadhi wa TFS, Prof Dos Santos Silayo, alisema hayo jijini Dodoma wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa kwa watumishi hao wapya, akiwataka kujiepusha na vitendo vya rushwa, kuzingatia weledi na kuwekeza katika ubunifu kwa ajili ya maendeleo ya kitaaluma na TFS kwa ujumla.
“Msitumie vibaya dhamana hii mliyopewa. Nendeni mkawahudumie watu. Heshimianeni na kushirikiana na epukeni tamaa kwa sababu inaweza kuwapeleka kwenye vitendo vya rushwa,” Prof. Silayo alisema.
Akifafanua, Kamishna huyo alisema ubunifu utasaidia kuongeza mapato ya nchi, akiwataka watumishi hao wapya kutumia vizuri rasilimali watakazokabidhiwa kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya uhifadhi.
Prof Silayo pia aliwataka watumishi hao kuwa wazalendo, kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia utu na heshima.
Kwa mujibu wake, sekta za misitu na nyuki ni muhimu katika kuhakikisha usalama wa chakula na uhifadhi wa mazingira, ndiyo maana TFS inahakikisha watumishi wake wanapata mafunzo ya kutosha ili kulinda rasilimali hizo.
Aliwataka watumishi hao wapya kuepuka matumizi yaliyopitiliza ya mitandao ya kijamii na ulevi, akisema mambo hayo yanaweza kuhatarisha ajira zao na kusababisha makosa yatokanayo na uzembe.
Alieleza kuwa watumishi hao wapya wanatoka katika kada mbalimbali, zikiwemo udaktari, uhandisi, misitu na ufugaji nyuki.
Kamishna huyo wa TFS alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kibali cha kuajiri watumishi hao wapya, akisema Wakala huo unatarajia kuajiri watumishi wengine hivi karibuni kwa lengo la kuongeza nguvu katika sekta hiyo ambayo ni muhimu kwa uchumi wa nchi na juhudi za uhifadhi.
Akizungumzia mafunzo hayo ya utambulisho, Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Emmanuel Kiboko, alisema yameandaliwa kwa makusudi ili kuwapa watumishi hao wapya fursa ya kuifahamu menejimenti ya Wakala, kupokea maelekezo na kuelewa namna ya kusimamia utekelezaji wake.
Kiboko aliwataka watumishi hao wapya kuwa tayari kufanya kazi popote watakapopangiwa ndani ya nchi, huku akiwashauri kwenda kuwatumikia wananchi kwa upendo na uadilifu.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mhifadhi Daraja la Tatu, Omega Shamakala, alisema watumishi hao wamekutanishwa baada ya kuhitimisha mafunzo yao ili kupatiwa mafunzo ya utambulisho yatakayowasaidia kuifahamu taasisi vizuri kwa kuwa wao ni wafanyakazi wapya.
“Kwa hiyo, tunamshukuru Mungu kwa kutufikisha hapa. Mchango wetu katika sekta ya uhifadhi, sisi kama wahifadhi, ni kuhakikisha kwamba tunaendelea kuzilinda rasilimali za misitu na nyuki, ambayo ni miongoni mwa majukumu yetu makubwa.”
Shamakala aliongeza kuwa kupitia nafasi yake kama Ofisa Uhusiano, atahakikisha taasisi hiyo inaendelea kuimarisha ushirikiano na umoja na wananchi pamoja na wadau wengine, akisema bila ushirikiano huo taasisi pekee haiwezi kufikia malengo yake.
Judith Pius, ambaye ni miongoni mwa watumishi wapya walioajiriwa na TFS, alisema atafanya kazi kwa bidii kuhakikisha rasilimali za misitu na nyuki zinahifadhiwa na kulindwa ipasavyo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.




❤️ Wasichana warembo na wenye hamu ya kimapenzi kutoka kote duniani wanakungoja; jiunge hapa …………………………………………………………………….……> https://da.gd/girls66