Mikakati yasukwa kupunguza ajali barabarani

DAR ES SALAAM: Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ayoub Mohammed Mahmoud, ameongoza kikao kazi cha baraza hilo kujadili hali ya usalama barabarani na mikakati ya kuimarisha usalama kwa watumiaji wa barabara.

Kikao hicho kimefanyika Dar es Salaam, kimejadili masuala mbalimbali ikiwemo mikakati ya kupunguza ajali na makosa ya barabarani, pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na taasisi zinazohusika na usalama na miundombinu ya barabara.

Aidha, kikao hicho kimejadili umuhimu wa kutumia takwimu za ajali katika kutathmini athari zake kiuchumi na kijamii, hatua inayolenga kusaidia katika kupanga mikakati madhubuti ya kuimarisha usalama barabarani.

Sambamba na hilo, Ayoub amewakumbusha viongozi wa madereva wa mabasi na malori, wamiliki wa vyombo vya usafiri pamoja na viongozi wa bodaboda kuhakikisha wanawasisitiza wanachama wao kuzingatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kuhusu mwenendo wa hali ya hewa.

Amesema ni muhimu madereva na watumiaji wengine wa barabara kuchukua hatua stahiki wakati wa kutekeleza majukumu yao, hasa katika kipindi ambacho hali ya hewa inaweza kuathiri usalama wa usafiri.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button