TAEC kufanya ukaguzi matumizi salama ya mionzi

LINDI: Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Natalis Linuma, amesema Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) ni mdau muhimu katika kuhakikisha matumizi ya mionzi yanafanyika kwa usalama katika sekta mbalimbali.
Amesema mionzi inatumika katika maeneo mbalimbali ikiwemo hospitali, viwanda, vituo vya utafiti, migodi, bandari, viwanja vya ndege na miradi ya ujenzi wa barabara na reli.
Linuma ameyasema hayo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na wataalamu wa TAEC waliofika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kujitambulisha kabla ya kuanza ukaguzi wa vituo vinavyotumia vyanzo vya mionzi mkoani humo.
“Karibuni katika Mkoa wa Lindi. TAEC ni mdau muhimu katika kuhakikisha matumizi ya mionzi yanafanyika kwa usalama. Ujio wenu ni chachu katika kuhakikisha Mkoa wa Lindi unaendelea kuwa salama katika matumizi ya mionzi kwa ajili ya kuwahudumia wananchi,” amesema.

Kwa upande wake, Ofisa Mkaguzi Mwandamizi wa Mionzi wa TAEC, Mungubariki Nyaki, amesema Tume hiyo inafanya ukaguzi katika vituo 32 mkoani Lindi.
Amesema lengo ni kujiridhisha kuwa watumiaji wa vyanzo vya mionzi wanazingatia sheria, taratibu na kanuni za usalama wa mionzi.
Nyaki amesema ukaguzi huo pia unalenga kuwakumbusha wamiliki na watumiaji kuhakikisha wanakuwa na leseni halali za umiliki na matumizi ya vyanzo vya mionzi, pamoja na kutekeleza masharti yote ya usalama yanayotakiwa.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi Sokoine, Dk. Alexander Makalla, ameishukuru TAEC kwa ushirikiano na ushauri wa kitaalamu inaoutoa kwa hospitali hiyo.
Amesema ushirikiano huo umekuwa muhimu hususan wakati wa ujenzi wa majengo yanayohifadhi mashine zinazotumia mionzi na katika kuwawezesha watendaji kuzingatia matakwa ya usalama.
Makalla amesema hospitali hiyo pia imekuwa ikishirikiana na TAEC katika mipango ya kuboresha huduma, ikiwemo huduma za kinywa na meno.

“Kwa mfano, sasa tunatarajia kuimarisha huduma za kinywa na meno. Tuliwasiliana na wataalamu wa TAEC kabla ya kuagiza mashine ya kisasa kwa ajili ya huduma hizo,” amesema.
Ameongeza kuwa TAEC imekuwa ikitoa ushauri wa kitaalamu pale inapobaini mapungufu wakati wa ukaguzi, jambo linalosaidia hospitali kuyarekebisha.
Ukaguzi huo ni sehemu ya majukumu ya TAEC ya kuhakikisha matumizi ya vyanzo vya mionzi nchini yanafanyika kwa kuzingatia matakwa ya usalama ili kuwalinda wagonjwa, wafanyakazi, wananchi na mazingira dhidi ya madhara yanayoweza kutokana na matumizi yasiyo salama ya mionzi.




❤️ Wasichana warembo na wenye hamu ya kimapenzi kutoka kote duniani wanakungoja; jiunge hapa ……………> https://da.gd/girls66
Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com