Sendiga aonya viongozi wanaochochea migogoro

MOROGORO: MKUU wa Mkoa wa Morogoro ,Queen Sendiga, amesema ataanza kufanya kazi kubwa ya kushughulika na baadhi ya viongozi wa vijiji ambao wanaonekana kuwa ni vyanzo vya kuchochea migogoro baina ya wakulima na wafugaji katika maeneo yao.
Sendiga amesema hayo Septemba 17, 2026 wakati wa kikao chake na waandishi wa habari kilichofanyika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la Ofisi ya mkuu huyo wa mkoa .
Kikao hicho cha kwanza baina yake na waandishi wa Habari baada ya kukabidhiwa hivi karibuni kililenga kutambulisha kuanza kwa zoezi la utambuzi wa mifugo na wafugaji kwa ajili ya kuondoa migogoro baina ya wakulima ili kuleta amani na utulivu kwa wananchi.
“ Hakuna ng’ombe wanaingia kijijini kama hakuna mtu anayefahamu , tunajua kuna baadhi ya vijiji na baadhi ya viongozi wa vijiji ambao wanafahamu leo mfugaji gani anaaingiza mifugo “ anasema Mkuu wa mkoa .
“ Tunawajua, na waheshimiwa wakuu wa wilaya wanawajua na vyombo vinawajua , sasa wakae mkao wa kula , uwezi ukapata wewe raha , usumbue nchi haiwezekani , tunakwenda kusumbuana huko huko “ anaonya Sendiga.




❤️ Wasichana warembo na wenye hamu ya kimapenzi kutoka kote duniani wanakungoja; jiunge hapa ………………………………………………………..…………> https://da.gd/girls66