Mji Kondoa yatumia milioni 154/- kuboresha sekta ya elimu

KONDOA, DODOMA: Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa, mkoani Dodoma, Said Majaliwa kwa kuwa serikali tayari imetumia takribani Sh milioni 154 kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Amelazimika kufafanua hilo wakati akikanusha taarifa zilizodai kuwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Hurumbi, iliyopo Kata ya Selia, wanasoma wanatumia miundombinu chakavu.

Majaliwa alisema hayo hivi karibuni wakati akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha picha za madarasa na vyoo chakavu katika shule hiyo.

Alisema taarifa hizo hazioneshi hali halisi ya miundombinu iliyopo shuleni hapo, kwa kuwa Serikali tayari imetumia takribani Sh milioni 154 kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Kwa mujibu wa Majaliwa, ujenzi wa miundombinu hiyo ulikamilika Desemba 2025, ukiwamo ujenzi wa madarasa matatu ya elimu ya awali, madarasa matatu ya shule ya msingi, matundu manne ya vyoo vya wanafunzi na matundu 12 ya vyoo.
“Kwa hiyo hakuna mwanafunzi anayesomea kwenye miundombinu chakavu, kwa sababu Serikali tayari imewekeza fedha katika kuboresha mazingira ya shule hii,” alisema.

Aidha, Majaliwa alisema Halmashauri ya Mji wa Kondoa imetumia Sh milioni nne kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya kujenga matundu mawili ya vyoo vya walimu, ikiwa ni sehemu ya hatua za kuboresha mazingira ya shule.

Majaliwa aliwataka waandishi wa habari kuhakikisha wanahakiki taarifa kabla ya kuzichapisha au kuzisambaza, akisema taarifa zisizothibitishwa zinaweza kupotosha umma kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Ni muhimu waandishi wa habari kutembelea maeneo husika, kuzungumza na mamlaka na kuthibitisha taarifa kabla ya kuzisambaza ili wananchi wapate habari sahihi.”
Alisisitiza kuwa taarifa kuhusu shule hiyo zinapaswa kuzingatia hali ya sasa ya miundombinu, ikiwamo madarasa, vyoo na tarehe ya kukamilika kwa miradi iliyotekelezwa.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button