Makonda ataka michezo itumike elimu utunzaji misitu

MOROGORO; WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema michezo inaweza kuwa nyenzo muhimu ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuhifadhi misitu na mazingira, kwani wanapoweza kuona na kunufaika na rasilimali hizo.
Makonda, amesema hayo Oktoba 3, 2026 wakati wa ziara yake eneo la mashindano ya Serengeti Rally of Tanzania 2026 katika Shamba la Miti Morogoro, ambapo pia alitembelea banda la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na kupata maelezo kuhusu shughuli za uhifadhi zinazotekelezwa na wakala huo .
Waziri Makonda amesema mashindano yanayofanyika katika mazingira ya misitu yanatoa fursa kwa wananchi kujifunza kwa vitendo kuhusu thamani ya misitu na umuhimu wa kuilinda.

“Ni jambo la kujifunza kwa kuona, ukijifunza kwa vitendo unapata fursa kubwa zaidi ya kuelewa,” amesema Makonda.
Makonda amesema kuwa misitu ina mchango muhimu katika maisha ya wananchi, ikiwemo kusaidia upatikanaji wa mvua na mazingira bora ya kuishi, hivyo jamii inapaswa kuendelea kunufaika nayo na kuzilinda rasilimali hizo.
Kwa kutambua umuhimu huo , amewahimiza Watanzania kuwa walinzi wa misitu kwa kutambua thamani yake na kushiriki kikamilifu katika kuilinda dhidi ya uharibifu.
“ Manufaa yanayotokana na misitu yanaweza kuendelea kupatikana iwapo rasilimali hizo zitatunzwa kwa kizazi cha sasa na kijacho,” amesema Makonda.
Kwa upande wake, Ofisa Utalii wa TFS, Salome Kivuyo amesema Wakala huo unaendelea kuwashirikisha wadau na wafadhili katika kuendeleza michezo ndani ya maeneo ya misitu kwa kuzingatia taratibu za uhifadhi.
Kivuyo amesema kuwa michezo hiyo ni pamoja na mbio za baiskeli, pikipiki na marathon, kwa lengo la kuunganisha michezo na uhifadhi wa mazingira.

“Tunawakaribisha wadau mbalimbali waje tushirikiane katika kuleta michezo ndani ya misitu yetu, ili kuwapa Watanzania fursa ya kufurahia michezo hiyo, huku wakijifunza, kutambua na kuthamini thamani ya misitu na umuhimu wa kuilinda,” amesema Kivuyo.
Akielezea mashindano hayo amesema yameandaliwa vema na kufanyika katika mazingira ya Shamba la Miti Morogoro, na kwa kuunganishwa michezo na uhifadhi kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ikiwa na kukuza michezo na utalii.
Kivuyo amesema kuwa Mashindano ya Serengeti Rally of Tanzania 2026 yanayofanyika Shamba la Miti Morogoro, linalosimamiwa na TFS, yamekuwa fursa ya kuunganisha michezo, uhifadhi, utalii na elimu ya mazingira.




Thiѕ is very іnteresting, Yоu’re a very skilled blogger.
I һave joined yoᥙr rss feed and look forward to seeking more
of your magnificent post. Aⅼso, I’ve shared yoսr site іn my social networks!
Visit mmy web blog :: singapore online math tuition
Gгeat article аnd straight tօ the point. I am not sᥙre іf this is actuaⅼly the
ƅest place to asҝ but ddo уou folks have any ideea wheгe to ցet
sone professional writers? Ꭲhank yοu 🙂
my site … math home tuition singapore 90
Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com
Constructing video sequences directly from written prompts simplifies rapid media prototyping. Creators who build videos from text prompts on wan 3 can experiment with story ideas without using complex software.
❤️ World hot and horny girls are waiting for you join here ………………..> https://tinyurl.com/2tdrwdpp