Ngumi za kisultani kupigwa safari ya beach

DAR ES SALAAM: Bondia Sultani Kiyoko ametamba kumtwanga  Fransic Nampumula wa Mbagala kwenye pambano la safari ya Beach linarotarajiwa kupigwa Oktoba 22, 2023, Rongoni Beach Kigamboni Jijini Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, wakati akiendelea na maandalizi Bondia Sultan Kiyoko amesema mazoezi anayofanya ni zaidi ya kucheza raundi sita.

“Nitakachofanya ni zaidi ya kucheza raundi sita walizo saini hivyo mpinzani afanye mazoezi ya kutosha ya kupokea kipigo cha aina yake siku hiyo.”amesema  Bondia Kiyoko

Saidi Omar ni mdau wa masumbwi ambaye ni shabiki wa Kiyoko amesema “damu zitamwagika ulingoni kwa mpinzani wao  baada ya kupokea kichapo kitakacho pelekea kutotamani kucheza ngumi maisha yake yote.”amesema.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button